Rais Kenyatta Amekutana Na Rais Biden Wa Marekani

Rais Uhuru Kenyatta ameweza kuandikisha  historia kwa kuwa rais  wa kwanza wa Kiafrika kukaribishwa na Rais Joe Biden katika Ikulu ya White tangu kiongozi huyo wa Marekani alipochukua madaraka mnamo Januari mwaka huu.

Ujumbe wa Kenya Ukiongozwa na rais Uruhu Kenyatta wakutana na rais Joe Biden katika ikulu ya White House Marekani

Katika mkutano huo wa kihistoria, Rais Biden alitangaza msaada wa serikali ya Marekani wa dozi milioni 17 zaidi za chanjo ya Covid-19 kwa Umoja wa Afrika.

Also Read
Wakaazi Wa Kasemeni Wapokea Fidia
Also Read
Ruto atakiwa kutowajibu wakosoaji wake.

Rais Kenyatta aliishukuru serikali ya Marekani kwa kuendelea kusaidia Kenya na bara la Afrika katika vita dhidi ya Covid-19, na alikaribisha mchango wa nyongeza ya dozi milioni 17 kwa AU akibainisha kuwa Afrika ilikuwa ikihangaika kupata chanjo za kutosha.

Also Read
Mbunge Badi Twalib Awataka Viongozi Wapwani Kuhubiri Umoja

Mbali na Covid-19, viongozi hao pia walijadili vita vya kimataifa dhidi ya ugaidi, mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na biashara na uwekezaji kati ya masomo mengine yenye faida kwa Kenya na Marekani.

  

Latest posts

Wafanyibiashara Katika Soko La Malindi Walalamikia Uchafu na Uvundo.

Sylvester Chibero

Wakenya Wametakiwa Kuwa Waangalifu Wakati Wanapoabiri Magari Msimu Huu Washerehe.

Sylvester Chibero

Tutashamiri Kwenye Mashindano Ya Mwaka Huu Ya Tong-IL Moo Do Asema Master Mwakio

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi