Walimu wametakiwa kuhakikisha wanawafunza maadaili mema wanafunzi wakiwa shuleni.
Akihutubia kongamano la chama cha walimu wakuu wa shule za upili KESSHA jijini Mombasa rais Uhuru Kenyatta amesema ni jukumu la walimu kuhakikisha kuwa wanafunzi wanakua raia wema kupitia mafunzo na maadili shuleni.
Kiongozi wa nchi amesema serikali imajitahidi kuhakikisha kuwa walimu wwanakua na mazingira bora ya kufanyia kazi pamoja na kuongezewa mishahara yao.
Wakati uo huo rais Kenyatta akigusia swala la siasa amewataka viongozi wanotafuta nyadhafa mbalimbali za uongozi nchini kuwa viongozi wanaoweza tatua matatizo ya wakenya sio kuongea bila kutoa suluhu.