Rais Uhuru Kenyatta wakati wowote kuanzia sasa anatarajiwa kukagua ujenzi wa Kituo kipya cha Mafuta cha Kipevu, Kipevu Oil Terminal unaoendelea kwenye bandari ya Mombasa.
Rais Kenyatta anambatana na waziri wa Masuala ya Nje wa Uchina, Wang Yi kukagua mradi huo.
Mradi huo unajumuisha magati manne ambayo yana urefu wa mita 770.
Pia kuna mabomba matano ambayo yalizikwa kina cha mita 26 ndani ya bahari ili kuhakikisha shughuli za kituo hicho zinaendelezwa pia kutatizwa.
Ujenzi huo ambao unaigharimu Mamlaka ya bandari kima cha shilingi bilioni 40 unatekelezwa na Kampuni ya Ujenzi ya China ya Communication Construction Company (CCCC).