Rais wa tatu mstaafu Mwai Kibaki amefariki akiwa na umri wa miaka 91.
Kifo chake kimethibitishwa na rais Uhuru Kenyatta katika ikulu ya Nairobi.
Rais Kenyatta amemuomboleza mtangulizi wake kama kiongozi ambaye alileta ukuaji wa kiuchumi , demokrasia na kuimarisha hali ya uchumi ya Wakenya.
amemkumbuka kwa jukumu lake la kupatikana kwa katiba mpya ya mwaka 2010 na kuongoza uidhinishaji wake.
Amesema kwamba bendera zote katika majumba ya umma , wizara na balozi zote duniani zitasalia nusu mlingoti hadi pale atakapozikwa.
Kibaki alihudumu kama rais wa tatu wa Kenya kati ya mwaka 2002 na 2013.
Aidha nchi hii itaandaa kipindi cha maombolezi kuanzia leo hadi siku ya mazishi ya Kibaki.
Aidha Rais Kenyatta aliagiza kwamba naibu wa rais, Jaji Mkuu, makatibu wa baraza la mawaziri, spika wa bunge la kitaifa, spika wa Seneti, Wanadiplomasia wa Kenya walio nje ya nchi na yeyote mwingine ambaye ameidhinishwa na sheria, hawatapeperusha bendera ya taifa kwenye misafara yao rasmi kuanzia leo hadi siku ambayo Kibaki atazikwa.