Rais Mteule Ruto Kukutana Na Viongozi Wa Mrengo Wa Kenya Kwanza

Rais mteule Dkt.William Ruto na naibu mteule wa rais Rigathi Gachagua wanatarajiwa kukutana na viongozi wote waliochaguliwa wa chama cha UDA pamoja na Kenya Kwanza kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliopita.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari mwenyekiti wa chama cha UDA Veronica Maina amesema wawili hao watakutana na magavana waliochaguliwa kupitia muungano wa Kenya Kwanza, pamoja na maseneta na wawakilishi wanawake katika makazi ya naibu rais huko Karen saa tatu asubuhi.

Also Read
Rais Dkt Ruto Ameyataka Mataifa Kushirikiana Kukabiliana Na Mabadiliko Ya Tabianchi Na Majanga Ibuka
Also Read
Wanabiashara wa samaki walalamikia kupanda kwa bei ya sambaki Mombasa

Dkt.  Ruto, ambaye ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais kwenye uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkubwa na kumshinda mpinzani wake wa karibu Raila Amollo Odinga. 

UDA inatarajiwa kuwa na idadi kubwa ya maseneta baada ya kushinda viti 24 ikilinganishwa na 23 vya muungano wa Azimio La Umoja One Kenya chini ya uongozi wa Raila Odinga.

  

Latest posts

Watoto Wanaotelekezwa Wako Hatarini Ya Kujiunga Na Makundi Ya Kihalifu Asema Hakimu Nabwana

Clavery Khonde

Rais aahidi kukomesha aibu ya njaa nchini

Joshua Chome

Mradi Wa Unyunyiziaji Mashamba Maji TanaRiver Waimarishwa

Ruth Masita

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi