Rais Uhuru Kenyatta ahudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais mpya wa Zambia

Rais Uhuru Kenyatta alikuwa miongoni mwa viongozi 10 wa mataifa ya Kiafrika wakati wa kuapishwa kwa rais mpya wa Zambia,Hakainde Hichilema, mjini Lusaka.

Hichilema mwenye umri wa miaka 59 aliapishwa kuwa rais wa 7 pamoja na makamu rais wake Bi. Mutale Nalumango kwenye hafla iliyoandaliwa katika uwanja wa michezo wa National Heroes.

Also Read
Rais aiondoa lawamani afisi yake dhidi ya mvutano kuhusu ugavi wa mapato kwa kaunti

Kwenye hotuba yake ya kwanza, rais Hichilema alisema serikali yake itatoa nafasi sawa kwa raia wote wa Zambia na akaahidi kuhakikisha raia wote wanafurahia uhuru wao kama ilivyoratibishwa kwenye katiba.

Rais Felix Tshisekedi wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambaye pia ni mwenyekiti wa Muungano wa Afrika na rais Lazarus Chakwera wa Malawi ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa shirika la maendeleo kusini mwa Afrika-SADC, waliongea kwa niaba ya viongozi wa mataifa ya kiafrika waliohudhuria na wakawapongeza raia wa Zambia kwa kufanya uchaguzi wa amani.

Also Read
Rais Uhuru akutana na Prince Charles katika makaazi ya Sandringham Uingereza
Also Read
Alikiba Azindua Rasmi Jina La Album Yake Mpya

Aliyekuwa rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo ambaye aliwakilisha jopo la wazee mashuhuri barani Afrika alisema Zambia imeonyesha kwamba bara Afrika sasa limekomaa na kwamba kunaweza kuwa na mpito wa amani wa kukabidhi mamlaka kutoka chama kimoja cha kisiasa hadi kingine.

  

Latest posts

Kiwango Cha Wateja Waliofurahia Huduma Za KRA Ndani Ya Miaka 3 Imeongezeka

Ruth Masita

HURIA Yalaumu Vyama Vya Kisiasa

Clavery Khonde

Wakaazi Kwale Waitaka Serikali Kushughulikia Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi