Rais wa Uganda Yoweri Museveni awaomba msamaha Wakenya kwa jumbe kutoka kwa generali Mohoozi

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewaomba msamaha wakenya pamoja na Rais Dkt. William Ruto kuhusiana na jumbe za kejeli katika mtandao wa kijamii wa twita zilizotumwa na mwanawe generali Muhoozi Kainerugaba dhidi ya Kenya.

Katika taarifa, rais Museveni akiwapongeza Wakenya kwa kuendesha uchaguzi mkuu wa amani mnamo mwezi Agosti mwaka huu, alimpongeza rais William Ruto kwa ushindi wake.

Also Read
Bunge laidhinisha makamishna wanne walioteuliwa kuhudumu katika tume ya IEBC

Museveni kupitia taarifa alisema amezungumza binafsi na rais William Ruto kuhusiana na suala hilo.

Also Read
Mashahidi Waombwa Kujitokeza Kumtetea Aliyebakwa

Museveni alisema kamanda huyo wa zamani wa majeshi ya nchi kavu alikosea kwa kuingilia masuala ya ndani ya Kenya.

Alisema nchi zenye uhusiano bora hutangamana kupitia muungano wa mataifa ya bara Afrika ama kupitia jumuiya ya Afrika Mashariki.

Also Read
Kushindwa Msambweni Haimaanishi BBI Imefeli Asema Raila

Alisema uamuzi wa kumpa madaraka Muhoozi ni kutokana na mchango wake nchini humo,ambao usingevurugwa na tukio la ukosefu wa heshima alioonyesha.

Aidha Museveni aliwaomba msamaha raia wa Kenya ambao huenda waliudhika kutokana na jumbe hizo za twita.

  

Latest posts

Mvurya Ataka Maafisa Wa Idara Na Mashirika Ya Serikali Kuhusu Maendeleo Zishirikishe Serikali Za Ugatuzi

Ruth Masita

Wanawake Wajasiriamali 450 Wanufaika Na Mafunzo Ya Kibiashara Mombasa

Ruth Masita

Mahakama yamwachilia mbunge wa Sirisia John Walukhe kwa dhamana ya shilingi milioni kumi

Joshua Chome

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi