Refa Sikazwe Awashangaza Wengi Kwa Kutamatisha Mechi Kabla Ya Dakika 90 AFCON

Taharuki ilitanda katika michuano ya kombe la mataifa barani Afrika, AFCON, nchini Cameroon, baada ya Mali kuicharaza Tunisia kwenye mechi iliyojawa na mshike mshike pale  refa aliyeiongoza mechi hiyo kupuliza kipenga kabla ya dakila 90 kumalizika.

Refa Janny Sikazwe kutoka Zambia, alikipuliza kipenga ikiwa ni dakika 89 na sekunde 42, hatua iliyopelekea Tunisia kuvunjika moyo walipokuwa wakijitahidi angaa kupata goli la ukombozi dhidi ya Mali ambao walikuwa na wachezaji 10 baada ya mshambulizi wao El Bilal Toure kuonyeshwa kadi nyekundu dakika 6 baada ya kuingia uwanjani.

Also Read
Wahamiaji sita wafa maji Tunisia
Also Read
CORONA yapungua Afrika yasema CDC

Hadi refa huyo anamaliza mchezo Mali ilikua kifua mbele bao moja kwa bila.

Baada ya mazungumzo na wakuu wa michuano hio mechi iliamuriwa kuendelea ili kutimiza dakika tisini.

Lakini ni Mali ndio ilirejea uwanjani lakini Tunisia walidinda kurudi uwanjani hivyo kuwafanya  Mali kushinda mechi hiyo.

Also Read
Mali Inasukumwa Kubuni Serikali ya Utawala wa Kiraia

Haijabainika iwapo hatua ya Tunisia ya kutorejea uwanjani itapelekea kuchukuliwa kwao hatua za kinidhamu na shirikisho la soka barani  Afrika CAF.

 

  

Latest posts

Wakenya Wapongezwa Kwa Kudumisha Amani

Clavery Khonde

Wiper Yaapa Kujiimarisha Zaidi Pwani

Clavery Khonde

Rais Mteule Ruto Kukutana Na Viongozi Wa Mrengo Wa Kenya Kwanza

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi