Naibu rais William Ruto amewahimiza wakazi wa kaunti ya Taita Taveta ambapo ameandaa makongamano ya umma kuwachagua viongozi watakaowafanyia maendeleo.
Ruto amesema muungano wa Kenya Kwanza una mipango makhsusi ya kubuni nafasi za ajira, kuboresha nyumba na kuongeza thamani ya sekta ya uchimbaji madini miongoni mwa sekta nyingine.
Ruto amesema mfumo wake wa kiuchumi wa kuwapa uwezo watu wa tabaka la chini unalenga kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kwa kuwapa mikono kwa riba nafuu.
Ruto anaandaa msururu wa makongamano ya kiuchumi huku akijipigia debe katika azma yake ya kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti mwaka huu.