RwandAir yapoteza mwelekeo Entebbe

Ndege ya abiria iliteleza na kutoka kwenye njia yake ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda Jumatano asubuhi.

Kwamujibu wa RwandAir tukio hilo lilitokana na hali mbaya ya hewa na kusema kuwa abiria wote na wafanyakazi wa ndege walishuka salama bila majeraha yoyote.

Aidha mdhibiti wa anga ametangaza kuwa ipo njia mbadla ya ndege kurukia inayofanya kazi kwa ajili ya ndege ndogo na nyepesi na kuwa juhudi zote zinaendelea ili kuondoa ndege kwenye ukanda wa kuruka na kutua ili njia kuu ya kuruka na kutua ndege irudi kutumika kikamilifu.

Gazeti la Daily Monitor nchini Uganda, limeripoti kuwa abiria 20 kati ya 60 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo wameratibiwa kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa kwa mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba.

Inaripoti kuwa tafrija ya kuzaliwa kwa Jenerali Kainerugaba ya kutimiza miaka 48 imepangiwa kufanyika Jumapili.

Jenerali Kainerugaba, ambaye pia ni kamanda wa majeshi ya nchi kavu, alichapisha ujumbe mtandaoni siku ya Jumatatu kwamba aliyekuwa Miss Rwanda atakuwa miongoni mwa wageni watakaohudhuria hafla hiyo.

  

Latest posts

Ujenzi Wa Nyumba Za Gharama Nafuu Wafaa Kufanywa Nje Ya Jiji Asema Thoya

Clavery Khonde

Tedros Adhanom Ghebreyesus Achaguliwa Tena Kuwa Mkuu Wa WHO

Clavery Khonde

Jurgen Klopp Achaguliwa Kama Mkufunzi Bora Wa Ligi Ya EPL

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi