Semi za chuki zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa humu nchini wakati wa kampeni za siasa ya mwaka huu huenda zikachochea wawekezaji kutowekeza humu nchini kutokana na wasiwasi wa kiusalama.
Haya ni kulingana na wakili Allan Nyange.
Katika mahojiano ya kipekee na pwani fm Nyange amesema kuwa wawekezaji huzingatia sana usalama wa biashara zao ndio waweze kuwekeza katika eneo flani na endapo wanasiasa hawatathibiti ndimi zao basi huenda wawekezaji wengi wakakosa imani ya kuwekeza humu nchini.
Aidha amesema kesi za uchochezi zinafaa kusikilizwa kwa haraka mahakamani ili watakaopatikana na hatia waadhibiwe kwa mujibu wa sheria.
Huku akidokeza kuwa kesi hizi pia kuna uwezekano wa kuzitatua nje ya mahakama kama mwenye kufanya makosa atakubali na kuomba msamaha.