Serikali Kuimarisha Kilimo Kwenye Shamba La Galana Kulalu

Waziri wa maji na unyunyuziaji Sicily Kariuki amesema kuwa serikali ya kitaifa iko kwenye mchakato wa kuuza shamba la ekari 10,000 la mradi wa chakula wa Galana na Kulalu katika kaunti ya Kilifi na Tana River.

Waziri huyo amesema wizara yake pamoja na ile ya hazina ya Kitaifa iko katika mchakato wa kutambua sekta binafsi ya humu nchini au nchi ya nje itakayoendeleza kazi hiyo baada ya Mamlaka ya Taifa ya unyunyuziaji (NIA) kukamilisha kuweka miundombinu ya msingi ya unyunyizi wa maji.

Also Read
IEBC Yapinga Madai Ya Wizi Wa Kura

Sicily Kariuki amesema kuwa wizara yake, kupitia NIA, iko katika hatua za mwisho za kuweka miundombinu  ya unyunyiziaji mashamba maji kwenye ekari 4,900 zilizosalia za shamba hilo kabla ya mradi huo kutolewa kwa sekta ya kibinafsi.

Also Read
Wakaazi wa Kwale wahimizwa kuzingatia kilimo cha bustani kukabiliana na njaa

Kariuki  ambaye aliandamana na mtendaji mkuu wa NIA Gitonga Mugami miongoni mwa maafisa wengine wakuu, alisema kuwa zabuni za biashara ya shamba hilo zitakuwa za kimataifa ili kuhakikisha kuwa sekta ya kibinafsi itakayomiliki inaendesha miradi kikamilifu.

Also Read
Wizara Ya Kilimo Imeanzisha Mikakati Yakuwasaidia Wakulima Nchini

Aidha waziri huyo aliwakashifu baadhi ya vigogo wa kisiasa nchini kwa madai kuwa serikali imeachana na ajenda Nne kuu kwa madai kuwa serikali inafanyia kazi ajenda zake zote.

  

Latest posts

Uungereza Yaahidi Kushirikiana Na Kenya Kukabili Korona

Clavery Khonde

Wakenya Wahimizwa Kuwatunza Wanao Dhidi Ya Biashara Ya Ngono

Clavery Khonde

Viongozi Wa Dini Kwale Waonywa Dhidi Ya Kujihusisha Na Siasa

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi