Serikali Ya Ethiopia Yawafukuza Maafisa wa Umoja wa Mataifa

Umoja wa mataifa umeelezea kushangazwa kwake na hatua ya kufukuzwa kwa maafisa wake wakuu saba na serikali ya Ethiopia.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa António Guterres alisema umoja wa mataifa unashauriana na serikali ya Ethiopia kwa matarajio kwamba maafisa hao wataendelea na kazi yao.

Also Read
Shughuli Za Bandari Kuimarika Baada Ya Kuzinduliwa Kwa Barabara Ya Nyerere-Mbaraki

Maelfu ya watu wameuawa na wengine zaidi ya milioni mbili kutoroka makaazi yao tangu waziri mkuu Abiy Ahmed alipoagiza msako wa kijeshi dhidi ya vikosi vya mikoa huko Tigray mwezi Novemba mwaka 2020.

Also Read
Wanahabari wawezeshwa kuwajuza wananchi kuhusu matukio ya uchaguzi

Miongoni mwa waliotimuliwa katika tangazo hilo lililotolewa jana ni pamoja na mkuu wa afisi ya umoja wa mataifa ya ushirikishi wa masuala ya kibinadamu-UNOCHA na mkuu wa hazina ya watoto ya umoja wa mataifa-UNICEF nchini Ethiopia.

Also Read
Otile Brown, Nviiri na Wasanii Wengine Wapoteza Nyimbo Zao Youtube

Hadi sasa bado haijabainika walikabiliwa na madai gani.

  

Latest posts

Kiwango Cha Wateja Waliofurahia Huduma Za KRA Ndani Ya Miaka 3 Imeongezeka

Ruth Masita

HURIA Yalaumu Vyama Vya Kisiasa

Clavery Khonde

Wakaazi Kwale Waitaka Serikali Kushughulikia Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi