Serikali Ya Kaunti Ya Kilifi Kuanza Kutoa Chanjo Ya Johnson and Johnson

Idara ya afya kaujnti ya Kilifi inalenga kuanza kutoa chanjo kwa mara ya kwanza za aina ya Johnson and Johnson pamoja na Faiza hivi karibuni.

Kulingana na afisa wa afya ya umma katika hosipitali ya rufaa kaunti ya Kilifi Erick Maitha, maafisa wa afya wanapokea mafunzo ya  jinsi watakavyo peana chanjo hiyo jijini Nairobi.

Also Read
Umaskini watajwa kuwa chanzo cha mimba za mapema Magarini

Akizungumza afisini mwake mjini Kilifi, Maitha amesema wakazi watapewa nafasi ya kujichagulia ni chanjo aina gani watakayopenda kuchanjwa.

Also Read
Wakaazi Wa Kilifi Watahadharishwa Dhidi Ya Mafuriko

Vile vile afisa huyo amesema kutokana na hamasa ambazo zimetolewa na washikadau mbalimbali kuhusu umuhimu wa chanjo hizo wakazi wengi wanajitokeza kuchanjwa.

Also Read
Waziri Magoha Aagiza Kufungwa Kwa Shule Nchini

Wizara ya afya nchini hivi leo imepokea zaidi ya  chanzo laki nane  aina ya Moderna kutoka nchini Marekani.

  

Latest posts

Kiwango Cha Wateja Waliofurahia Huduma Za KRA Ndani Ya Miaka 3 Imeongezeka

Ruth Masita

HURIA Yalaumu Vyama Vya Kisiasa

Clavery Khonde

Wakaazi Kwale Waitaka Serikali Kushughulikia Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi