Serikali imehimizwa kubuni tume maalum yakushughulikia mishahara na mahitaji ya madaktari na wauguzi.
Katika mahojiano ya kipekee na pwani fm mwaniaji wa kiti cha ubunge katika eneo bunga la Mwatate Christopher Mwambingu amehoji kuwa ipo haja ya tume hio kubuniwa ili kutatua mzozo wa migomo ya mara kwa mara ya wahudumu wa afya katika nagzi ya kaunti.
Mwambingu anasema serikali za kaunti zinafaa kusimamia swala la miundomsingi pekee katika sekta ya afya na kuiwacha serikali kuu kuwalipa mishaahara wahudumu wa afya.
Wkati uo huo Mwambingu amesema kuwa viongozi wamekosa kuingilia kati kuhakikisha kuwa serikali kuu inatoa mgao kwa kaunti kwa wakati unaofaa akisema kuwa hali hio imechangia pakubwa kwa kuchelewa kwa mishahara ya wafanyikazi wa serikali za kaunti.
Amesema baadhi ya wawakilishi wadi, wabunge na maseneta kwa njia moja ama nyengine wamefeli kuisukuma wizara ya fedha kuwachilia mgao wa serikali zakaunti kwa wakati.