Wizara ya elimu imefanyia marekebisho mkakati wa kitaifa kuboresha viwango vya elimu kwa minajili ya kuimarisha utoaji wa huduma katika taasisi za masomo.
Waziri wa elimu George Magoha amesema kuwa mkakati huo utaimarisha matokeo ya masomo kwa kuzingatia ushahidi na utendakazi bora.
Prof. Magoha alisema kuwa kwa miaka mingi, mtindo wa kukagua taasisi za masomo ya chekechea haujakuwa ukisaidia kuboresha ubora wa masomo, utoaji wa huduma na kuridhisha wadau husika.
Alisema mkakati huo mpya utatambua na kujumuisha vifaa katika kiwango kimoja kilichoboreshwa.
Mkakati huo unaanzisha vifaa ambavyo vitatumika katika ukaguzi wa kibinafsi na ule wa kutoka nje.
Aidha mchakato huo utatumia teknolojia ya habari na mawasiliano ambapo shule zote zitatarajiwa kushiriki.