Mwenyekiti wa baraza la kitaifa la ushauri kwa waislamu KEMNAC Sheikh Juma Ngao amemtaka rais Uhuru Kenyatta kuzingatia swala la kuwateuwa mabalozi wa kiislamu katika mataifa ya kiislamu.
Akizungumza katika siku ya mwisho ya warsha ya baraza hilo lililowaleta wahubiri wa kiislamu kutoka maeneo mbalimbali nchini katika hoteli moja hapa Mombasa,Ngao amesema kuna haja ya marekebisho hayo kufanywa ili matakwa ya maswala ya kiislamu yaweze kuwa rahisi kujadiliwa.
Kuhusu swala la uchumi samawati, Ngao amewataka waumini wa dini ya kiisalamu na wananchi wa Pwani kwa jumla kusoma lugha mbalimbali ili kuwa katika nafasi ya kuajiriwa katika sekta ya uchumi wa baharini katika nchi za nje.
Kwa upande wa maswala ya kisiasa mwenyekiti huyo wa Kemnac amesema kuwa kama baraza watafuata nyayo za rais Uhuru Kenyatta kwa kumuunga mkono kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kunyakua urais katika uchaguzi mkuu ujao.