Shirika la WWF-Kenya na wahisani wake wachangisha mitambo ya kuchakachua taka za plastiki kuzifanya taka mali

Shirika linalojihusisha na utunzaji wa mazingira la kimatafa la world wide fund for nature humu nchini  likishirikiana, wakfu wa Coca Cola na serikali ya kuanti ya Mombasa na wadau wengine wa utunzaji wa mazingira limevizawadi vikundi vitatu vya kijamii vinavuyojihusisha na utunzaji wa mazingira, kwa mitambo mitatu ta kuokota na uchakachuaji wa taka za plastiki.

Ni mitambo ya iliyogharimu zaidi ya milioni kumi (10m) kwa lengo la kuzibadilisha taka za plastiki kuwa taka mali.

Akiongea na wanahabari hapa mjini Mombasa kwenye sherehe ya kuzawadi mitambo hiyo afisaa mkuu wa utunzaji wa mazingira katika shirika la WWF hapa nchini Jackson Kiplagat anasema bado taka za plastiki zinasalia kuwa kero la uchafuzi wa mazingira nchini na duniani, akisema kama shirika wako mbioni kuja na mbinu ya kuyanusuru mazingira kupitia kuzibadilisha taka zote za plastiki kupitia kuzifanya taka kuwa vyanzo vya ajira miongoni mwa jamii.

Also Read
Kituo Cha Kukabiliana Na Magonjwa Ya Mmea Wa Mhogo Chazinduliwa Kilifi
Mountain garbage in Municipal landfill for household waste.

Aidha Kiplaga ameitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kuja na sheria madhubuti ya utunzaji wa mazingira pamoja na kuviwezesha vikundi vya jamii vilivyopo na wawekezaji wengine ambao wamejitokeza kuzibadilisha taka za plastiki hadi kwenye matumizi mengine ili kudhibiti utapakaaji wa taka hizo kwenye mazingira hasa maeneo ya baharini.

Also Read
Kesi Ya BBI Kuskizwa Januari

Waziri wa mazingira kaunti ya Mombasa Daktari Godffery Nato anasema kaunti ya Mombasa imejitoleo kuvipa vikundi vyote vya kijamii ambavyo viko tayari kuwekeza katika ukusanyaji wa taka ili kuzibadilisha taka katika  matumizi mengine.

Nato akiongeza kwamba vitundi hivyo vinachukuliwa kama wadau wakuu katika wizara ya mazingira na kwamba pia kaunti itajishughulisha kwa karibu kuvitaftia soko.

Also Read
Kenya yaungana na ulimwengu kusherekea siku ya mabaharia

Wanachama wa vikundi vilivyofaidika na mradi huu aidha wamelilimbikizia sifa shirika la WWF kwa juhudi zake za kuyawezesha makundi haya kujenga ajira miongoni mwa wakenya na kuwawezesha pia kuchangia katika kampeni ya kupigana na uchafuzi wa mazingira, wakiapa kwamba kila taka zilizoko kwenye mazingira zinaweza badilishwa zikajenga ajira za maelfu ya makundi ya vijana na kinamama katika jamii.

  

Latest posts

Nitaiboresha Idara Ya Usalama Kaunti Ya Mombasa Asema Abdullswamad Shariff Nassir

Clavery Khonde

Mpango Wa Wanawake Wazinduliwa Kwlae

Clavery Khonde

Waziri Magoha Aahidi Uimarishwaji Zaidi Wa Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi