Mashirika ya kijamii katika kaunti ya Taita Taveta yamewarai wanasiasa kutoingiza siasa katika maswala nyeti ya ardhi hali inayoweza kuibua taharuki miongoni mwa wakaazi.
Yakiongozwa na shirika la Taita Taveta Human Rights watch, mashirika hayo yamekashifu hatua ya magavana Granton Samboja na gavana wa Kajiado Joseph Olelenku kwa kusuluhisha mpaka baina ya kaunti hizo mbili, bila kuwahusisha kikamilifu wakaazi wa Njukinyi, hali inayoibua uhasama baina ya jamii ya wafugaji wa wakulima wa njukinyi.
Haji Mwakio Mwakio ni mwenyekiti wa shirika hilo kaunti ya Taita Taveta.
Kadhalika wamewataka wanasiasa kufanya maamuzi umhimu kwa mjibu wa sheria kwa kuhusisha kila mshikadau husika.
Haya yanajiri huku mkulima mmoja mkaazi wa njukinyi akiendelea kuuguza majeraha ya shingo baada ya kukatwa na panga Kufuatia mzozo wa malisho shambani kwake.