Sonko Mashakani

Mgombea wa kiti cha ugavana wa Mombasa kupitia chama cha Wiper Mike Mbuvi Sonko, bado itamlazimu kufuata Sheria kabla ya kuidhinishwa kugombea wadhfa huo.

Hii ni baada ya mkurugenzi mkuu wa mshtaka ya umma nchini Noordin Hajj na mwenzake wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi Twalib Mbarak, kukariri kwamba gavana huyo hafai kushikilia afisi yoyote ya umma.

Also Read
Barabara Ya Makupa Causeway Kufungwa

Hajji  amesema  kwamba Sonko anahujuma katiba kwa kutoroka kaunti ya Nairobi alikobanduliwa kama gavana kwa tuhma za ufisadi, na kukimbilia kaunti ya Mombasa kugombea wadhfa uo huo.

Also Read
Twaha: Tusiwachague Viongozi Kwa Misingi Ya Vyama Bali Utendakazi Wao

Kwa upande  wake afisa mkuu mtendaji wa tume ya kupambana na ufisadi EACC Twalib Mbarak, anadai kuwa Sonko anakabiliwa na kosa la kutoroka jela, hivyo kuwarai wakaazi wa Mombasa kuwa na busara wanapochagua viongozi.

Also Read
Achani ahimiza serikali kuongeza Mgao wa fedha kwa kaunti

Wawili hao wameyasema hayo hapa Mombasa, wakati wa kongamano la viongozi wa mashtaka ya umma kutoka bara la  Afrika.

  

Latest posts

Waziri Magoha Aahidi Uimarishwaji Zaidi Wa Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Pwani Wahamasisha Wenzao Kuhusu Amani

Clavery Khonde

Viongozi Fulani Hawataki Sonko Awe Kwenye Debe Asema Mbogo

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi