Tedros Adhanom Ghebreyesus Achaguliwa Tena Kuwa Mkuu Wa WHO

Tedros Adhanom Ghebreyesus wa Ethiopia amechaguliwa tena kuwa mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa muhula wa pili wa miaka mitano.

Matokeo ya kura ya siri yalikuwa ni utaratibu kwa vile alikuwa mgombea pekee.

Akifungua Mkutano wa 75 wa Afya Ulimwenguni huko Geneva, Dk Tedros, ambaye ameongoza mwitikio wa ulimwengu dhidi ya janga la Covid, alisema virusi vya corona vimeubadili ulimwengu, na kuwaacha wengi bado wanateseka.

Also Read
Wazazi Wametakiwa Kujukumikia Maadili Ya Watoto Wao

Akiyazuia machozi alipokuwa akizungumza, pia alitoa wito wa kukomeshwa kwa vita, ambayo alisema “inatikisa na kuvunja misingi ambayo jamii ziliisimamia”.

Alikumbuka uzoefu wake wa kwanza kama mtoto wa vita nchini Ethiopia, ambayo inakabiliwa tena na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe katika eneo lake la kaskazini la Tigray, ambako ni asili yake.

Also Read
Membe kupeperusha bendera wa chama cha ACT huko Tanzania

Mkuu huyo mwenye umri wa miaka 57 amekuwa katika mzozo na serikali ya Ethiopia baada ya kumshutumu kwa kuunga mkono vikosi vya Tigray – tuhuma ambayo ameikanusha hapo awali.

Also Read
Baadhi Ya Wakenya Wakwepa Utumiaji Wa Daraja La Liwatoni

Alikuwa Waziri wa Afya wa Ethiopia – ambapo alipokea sifa kwa juhudi zake za kudhibiti magonjwa kama vile malaria na UKIMWI – na waziri wa mambo ya nje kabla ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kuongoza WHO mwaka 2017.

 

  

Latest posts

Ofisi Ya Msajili Yawashirikisha Washikadau Kwenye Msafara Wa Amani Pwani

Ruth Masita

Nigeria yazikataa digrii za Ukraine

Tima Kisasa

Nzai Aeleza Nia Ya Kuimarisha Viwango Vya Elimu Jomvu

Ruth Masita

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi