Thoya Azungumza Azma Yakuleta Mabadiliko Ya Uongozi Mombasa

Mgombea mwenza wa ugavana kaunti ya Mombasa kupitia chama ODM Francis Thoya amesema watakabiliana na  kumaliza mizozo ya ardhi kaunti ya Mombasa endapo watachaguliwa kuiongoza kaunti ya Mombasa.

Katika mahojiano na Pwani fm Thoya anasema yeye ndiye aliyekuwa muasisi mkuu na mzinduzi wa ardhi za makaazi kaunti ya Mombaza ambazo anasema sasa zinasubiri tu kupata hati miliki.

Also Read
Spika Wa Bunge La Tana River Atimuliwa

Thoya anasema kwa mradi wowote wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu unahitajika kufanyika nje ya mji wa Mombasa ili kulifungua jiji la Mombasa ili kumaliza tatizo la mfumo wa utoaji wa maji taka katika sehemu za mji.

Also Read
Watu 7,553 Wamechanjwa Dhidi Ya Korona Mombasa

Aidha amekemea vikali wazo la kuhamisha utendaji kazi wa bandari ya Mombasa hadi katika eneo la Naivasha akisema hili lilipunja zaidi uchumi wa eneo hili.

Kuhusu   uwepo wa Dongo kundu economic zone Thoya anasema endapo wataingia uongozini watahakikisha vijana wamepokea mafunzo ya kujiandaa na ajira zitakazopatikana ndani ya mradi huo.

Also Read
Mkufunzi Firat Anapendelea Kuendelea Kuifunza Harambee Stars

Akijibu masuali ya wasilikizaji, Thoya amekubali kwamba kuna kuna matatizo mengi ndani ya kitengo cha inspectorate ambacho kimezua lalama nyingi miongoni mwa wananchi, akisema ni lazima kutakuwa na mabadiliko makubwa ikiwemo mafunzo ya maasifa wa inspectorate ili kumaliza uozo uliodumu ndani ya idara hiyo.

 

  

Latest posts

Ofisi Ya Msajili Yawashirikisha Washikadau Kwenye Msafara Wa Amani Pwani

Ruth Masita

Nzai Aeleza Nia Ya Kuimarisha Viwango Vya Elimu Jomvu

Ruth Masita

WRC Safari Rally Kuandaliwa Naivasha

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi