Timu Ya Morocco Yawasili Yaounde Kwa AFCON Na Vyakula, Vitanda Na Walinzi Wao

Kuwasili kwa Morocco kwa makala ya 33 ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon kumezua taharuki katika mji mkuu, Yaounde katika muda wa saa 72 zilizopita.

Timu hio inayojumuisha jumla ya  watu 86 wakiwemo wachezaji 28, wafanyakazi wa kiufundi na wa utawala walitua Yaounde siku ya Jumapili, wakiungana na timu za Ethiopia, Sudan na Zimbabwe, ambao waliwasili nchini Cameroon  mapema na kukita kambi kabla ya michuano huo iliopangwa kuanza Jumapili.

Also Read
Bingwa Mtetezi Algeria Atemwa Nje Ya AFCON

Ujio wa Simba wa Atlas hata hivyo haujakuwa gumzo la jiji hilo kutokana na ukweli kwamba walifika mapema, lakini kwa sababu timu imekuja na tani za chakula, wapishi, magodoro, vitanda na wafanyakazi wa hoteli kufanya kazi katika makazi yao ya muda mjini Yaounde.

Also Read
Kilio cha haki: Wakili atoroka na fedha za mteja wake aliyeshinda kesi ya ajali

Gazeti la kila siku la Morocco, Al Ahdath Al Maghribia liliripoti kwamba Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (FRMF) limechukua uamuzi wa kuepuka kuambukizwa kwa wachezaji wao na virusi vya korona.

Shirikisho hilo limehakikisha vyumba na vyumba vingine katika hoteli ya timu hiyo huko Yaounde viko sawa  huku vitanda na mablanketi yamebadilishwa na yale yanayosafirishwa kutoka Morocco.

Also Read
Kaunti ya Kwale kujenga kituo cha kutibu waraibu wa dawa za kulevya

Wafanyikazi wa hoteli walio na mawasiliano ya moja kwa moja na wachezaji wamebadilishwa na wale pia waliosafirishwa kutoka Morocco, wakati maajenti wa usalama pia wameletwa.

  

Latest posts

Gor Mahia Wapiga Kalamu Harrison na Benchi Lake La Kiufundi

Clavery Khonde

Sportpesa Yatoa Vifaa Vya Matibabu Kilifi

Clavery Khonde

Hospitali Za Kibinafsi Kukataa Huduma Za NHIF Mwezi Ujao

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi