Timu Za Denmark Na Swabrina Zashamiri Kwenye Mashindano Ya Rashid Abdallah Super Cup

Kilabu za Denmark fc na Swabrina Fc ndio mabingwa wa mashindano ya Rashid Abdallah super cup.

Denmark ilitawazwa mabingwa baada ya kuitandika Lazium mabao 5-4 kupitia mikwaju ya matuta baada ya timu hizo mbili kutoka sare ya kufungana bao 1-1 katika muda wa kawaida wa dakika tisini.

Also Read
Ushindi dhidi Comoros kuipa harambee stars million 15

Denmark iliweza kutuzwa nzumu 20, seti ya jezi, mipira miwili na hundi ya shilingi laki moja.

Swabrina Queens waliwarindima  kinadada wa Kombani Ladies 1-0.

Mwaasisi wa mashindano hayo Rashid Abdallah aliweka wazi kuwa mashindano hayo ni ya kuleta utangamano na umoja baina ya wakaazi wa Kwale na eneo Zima la Pwani huku akipinga madai kuwa ana nia ya kujitosa kwa siasa.

Kwa sasa nia yangu ni kuhakikisha hawa watu wa Waa ambayo ni sehemu niliyozaliwa , kulelewa na kucheza mpira wanakua wenye kuishi kwa umoja na kupendana kuhusu mambo mengine kwa sasa si mhimu. Alisema Abdallah.

Abdallah aliongeza kuwa mwaka ujao pia mashindano hayo yataandaliwa huku akiahidi kuwa atayanogesha zaidi.

Also Read
Biden kudhibiti wahamiaji wa Mexico na Guatemala
Also Read
Raila Amuomboleza Magufuli

Aidha aliwashukuru wadhamini wote kwa kuhakikisha mashindano hayo yanafana.

Wakati huo huo mwaasisi huyo aliwashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi kuzishangilia timu zao.

  

Latest posts

Gor Mahia Wapiga Kalamu Harrison na Benchi Lake La Kiufundi

Clavery Khonde

Sportpesa Yatoa Vifaa Vya Matibabu Kilifi

Clavery Khonde

Hospitali Za Kibinafsi Kukataa Huduma Za NHIF Mwezi Ujao

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi