Trump Ampiga Kalamu Afisa Wa Ngazi Za Juu Aliyepinga Madai Ya Wizi Wa Kura

Rais wa Marekani Donald Trump amesema amemwachisha kazi afisa wa ngazi za juu wa uchaguzi aliyepinga madai ya rais huyo kwamba uchaguzi wa urais nchini humo ulikumbwa na wizi wa kura.

Also Read
Mwanaharakati wa maendeleo Magarini Douglas Kudundi anasema umaskini unasababisha kuongezeka kwa visa vya uhalifu

Afisa mkuu wa shirika la kukabiliana na uhalifu wa kimtandao nchini humo Chris Krebs aliachishwa kazi kufuatia kile Trump alichotaja kuwa madai yasiyo ya kweli kuhusu uadilifu wa uchaguzi huo.

Also Read
Viongozi Wazidi Kutuma Risala Za Rambi rambi Kwa Familia Ya Chidzuga

Trump amekataa kukubali kushindwa kwenye uchaguzi huo na ametoa madai ambayo hayajathibitishwa kwamba ulikumbwa na wizi mkubwa wa kura.

Maafisa wa uchaguzi hata hivyo wamekanusha madai hayo. Krebs ndiye afisa wa serikali kuachishwa kazi hivi majuzi kufuatia kushindwa kwa Trump. Waziri wa ulinzi Mark Esper pia aliachishwa kazi huku kukiwa na tetesi kwamba Trump alitilia shaka uaminifu wake. 

  

Latest posts

Uteuzi Wa Karua Wapongezwa Na Wanawake

Clavery Khonde

Raila Amteua Martha Karua Kama Mgombea Mwenza Wake

Clavery Khonde

Wapwani Wahimizwa Kuunga Mkono Cha Cha PAA

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi