Wanachama wa bunge la kaunti ya Taita Taveta sasa wanashinikiza serikali ya kitaifa kuwapatia kiwango cha fedha zinazotoka katika mbuga ya Tsavo ili kujiendeleza.
Wakiongea katika eneo bunge Wundanyi wawakilishi hao wanasema wakati umefika kwa kaunti zinazopakana na mbuga ya Tsavo kupata mapato moja kwa moja.
Christopher Mwambingu ni mwakilishi mteule katika bunge la kaunti ya Taita Taveta.
Kadhalika wamekashifu shirika la wanyamapori chini ya usingizi wa waziri Najib Balala kwa kutowajibikia swala la fidia kufuatia hasara, majeraha na pia vifo vya wakaazi vinavyosababishwa na wanyamapori miaka minane sasa tangu sheria ya wanyamapori kupitishwa.