Wakazi wa eneo la Kavunzoni wadi ya Bamba kaunti ya Kilifi wamepata afueni baada ya mradi wa samaki kukamikilika na kuanza kutumika .
Kulingana na wakazi wa hao hali ya umasikili eneo hilo utapungua baada ya taasisi ya utafiti wa uvuvi na samaki KEMFRI kutoa mafunzo kwa wakazi hao jinsi ya kufanya miradi ya samaki maeneo kame.
Wakiongozwa na Robert Chengo na Stephen Fondo wanasema wataanza kufanya miradi ya unyunyiziaji mashamba ili waweze kupata chakula zaidi kutoka kwa maji ya kisima.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa uvuvi na samaki KEMFRI James Njiru anasema wanaendeleza utafiti kwa sehemu kame ili wakazi waweze kufanya miradi ya uchumi wa samawati.
Aidha Njiru amewataka wakazi wa sehemu hizo kuhakikisha hawategemi kilimo cha ufugaji wa mifugo pekee na kufanya ukulima wa samaki.
Mradi huo ulifadhiliwa na shirika ka KITANDA kutoka Ubelgiji.