Uhaba wa wahudumu wa afya yatatiza Zimbabwe

Madaktari nchini Zimbabwe wamesema kuwa nchi hiyo inakabiliwa na mzozo kutokana na uhaba wa wahudumu wa afya huku visa vya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 vikianza kuongezeka.

Dakta Rashida Ferrand, ambaye ni mtaalamu wa magonjwa kwenye hospitali kuu ya umma katika jiji kuu la nchi hiyo Harare, aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kwamba madaktari na wauguzi ni wachache mno kutokana na mgomo wa wahudumu wa afya ulioanza kabla ya janga hilo na vile vile uhaba wa vifaa vya kujikinga.

Zimbabwe imenakili takriban visa elfu-4 vya virusi vya Corona na vifo 70 ambavyo vimethibitishwa, lakini madaktari wanasema huenda idadi hiyo ni kubwa.

  

Latest posts

Malawi yamuomba Tyson kuwa balozi wake wa bangi

Tima Kisasa

UNESCO yaamua Kiswahili kuadhimishwa duniani kila tarehe 7 mwezi wa Julai

Tima Kisasa

Mataifa ya Asia Yaongoza Katika Uchafuzi wa Hewa Duniani

Ibrahim Nyundo

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi