Uingereza Ndani ya Fainali.

Timu Uingereza Imefuzu  finali ya dimba la Euro kwa mara ya kwanza katika historia yao baada ya bao la ukombozi la Harry Kane katika muda wa ziada uliyowafanya washinde 2-1 dhidi ya Denmark.

Timu ya Uingereza ilifungwa bao la kwanza katika mashindano hayo kupitia mchezaji Mikkel Dammsgard aliyefunga bao murwa iliyowashangaza mashabiki zaidi ya 60000 ndani ya uwanja wa Wembley.

Lakini muingereza alitikisa nyavu baada ya dakika tisa kupitia pasi laini kutoka kwa mchezaji Bukayo Saka ambapo mchezaji Simon Kajaer alijifunga.

Katika kipindi cha muda wa ziada mchezaji wa Manchester city Raheem Sterling aliwashindia Timu ya Uingereza penanti kwani alijaribu kupenya kati ya wachezaji wa Denmark nao wakambwaga penanti hiyo ilipewa mfungaji bora katika kikosi chao ila mlinda lango Kasper Shmeichel alitema mkwaju ule ila akawacha nyavu wazi ndipo Harry Kane akalitikisa.

Je ni nani atakalibeba dimba hili la euro Muitaliano au Muingereza? 

  

Latest posts

BETIKA  yawatuza wachezaji waliofana National super league

Ken Wekesa

ODM Yamteua Mohammed Hamid Kama Mwenyekiti Wa Tawi la Mombasa

Ruth Masita

Wafanyabiashara wa Kanda ya Afrika Mashariki Walalamikia Kupanda kwa Bei ya Mafuta Nchini

Ruth Masita

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi