Serikali ya kaunti ya Mombasa inafaa kufanya mpangilio mpya wa ujenzi na kuendeleza sehemu za nje ya katikati mwa jiji la Mombasa.
Haya ni kwa mujibu wa mgombea mwenza wa ugavana kupitia chama cha ODM kaunti ya Mombasa Francis Thoya.
Akizungumza na Pwani fm Thoya anasema kuwa katikati mwa jiji la Mombasa hakuna tena nafasi ya upanuzi na ujenzi wa nyumba za gharama nafuu akisema ili kuafikia ruwaza hii ni lazima mkakati wa kujenga nyumba nje ya jiji ili kuleta maendeleo kwa wakaazi wanaoishi vitongojini kaunti ya Mombasa.
Thoya anasema wakiunda serikali ya kaunti ya Mombasa watalitimiza hili na hawana nia ya kufurusha watu katikati mwa jiji la Mombasa.