Ujio wa chanjo dhidi ya korona humu nchini umetajwa kuwa huenda ukaimarisha sekta ya utalii wa humu nchini.
Akizungumza huko Shimoni kaunti ya Kwale wakati wa sherehe za kuadhimisha siku ya wanyamapori duniani katibu wa utawala katika wizara ya utalii Joseph Boinet amesema ujio huo utasaidia kuimarisha sekta hio.
Boinet aidha ameridhishwa na shirika la wanyamapori kwa kuhakikisha kuwa uwindaji haramu umepungua kwa asilimia kubwa humu nchini huku akisema kuwa uwindaji wa vifaru mnamo mwaka jana ulipungua kwa kiasi kikubwa.
Maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika kote nchini ambapo pia wakenya wamehamasishwa kuhusu madhara ya uwindaji haramu.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni umuhimu wa misitu katika maisha ya binadamu.
previous post