Ukataji wa Mikoko Wasababisha Kupungua Kwa Samaki Mombasa

Wakaazi wa moroto mjini Mombasa walalamikia kupungua kwa miti aina ya mikoko baharini kutokana na kukatwa kwa mikoko hiyo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Also Read
Tume ya mawasiliano yaanzisha mtambo mpya wa kiteknolojia kutambua mawimbi ya vituo vya redio

Wavuvi katika eneo hilo wanasema kuwa hali hiyo imepelekea kupungua kwa samaki na kuongezeka kwa mawimbi yasiyoweza kudhibitiwa kwani mikoko husaidia sana kudhubiti mawimbi makali.

Karisa Chengo mmoja wa wavuvi katika eneo hilo anasema kuwa swala la ukataji wa miti kumesababisha kuadimika kwa samaki hali ambayo inawaathiri kimaisha kwani wengi wao hutumia bidhaa ya samaki kujipatia kipato.

Aidha baadhi ya wavuvi wanasema kuwa ujenzi unaofanyika kwenye fuo za bahari pia umesababisha kuppotea kwa bidhaa hiyo muhimu ya samaki.

  

Latest posts

Kaunti ya Kilifi yaanza uboreshaji wa huduma za afya

Joshua Chome

Bunge lajadili hotuba ya rais huku mseto wa hisia ukiibuka kutoka kwa pande mbili

Joshua Chome

Rais wa Uganda Yoweri Museveni awaomba msamaha Wakenya kwa jumbe kutoka kwa generali Mohoozi

Joshua Chome

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi