Ukosefu wa nafasi za ajira umetajwa kama sababu kuu ya vijana wengi kutumiwa kiholela na wanasiasa kuzua rabsha kwenye mikutano ya wapinzani wao.
Katika mahojiano ya kipekee na pwani fm naibu wa walio wengi katika bunge la vijana kaunti ya Mombasa Omar Chai ameweka wazi kuwa ukosefu huo wa ajira umesababisha vijana wengi kupewa pesa na wanasisa kusababisha mvutano kwenye mikutano ya siasa.
Aidha anasema ahadi za wabasiasa ambazo wakati mwingi hazitimizwi pia zimechangia kwa asilimia kubwa kuwashawishi vijana kukubali kuujingiza kwenye mirengo ya siasa bila kujali kama hawatanufaika.
Kwa upande wake James Ruwa kiongozi wa vijana Bamburi amesema kuwa ukosefu wa ufahamu wa kutosha kuhusu uongozi na nafasi za kazi pia imechangia kwa vijana kujitosa kwa makundi yakisiasa.