Wakili wa haki za binadamu Amal Clooney amezitaka nchi kukusanya na kuhifadhi ushahidi wa ukatili nchini Ukraine.
Akizungumza katika mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini New York siku ya Jumatano, alisema: “Ukraine leo ni kichinjio.”
Pia alisema anahofia wanasiasa watakengeushwa na mambo mengine na kusahau yanayoendelea katika mzozo uliopo.
Clooney ni mmoja wa jopo kazi la kimataifa la kisheria linaloishauri Ukraine kuhusu kupata haki kwa wahasiriwa wa uhalifu wa kivita.