Leo Kenya inaungana na ulimwengu kusherehekea siku ya wauguzi duniani.
Siku ya kimataifa ya mauguzi huadhimishwa kila mwaka tarehe 12 Mei kwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa uuguzi wa kisasa, Florence Nightingale, lakini pia kuwaheshimu wauguzi kama rasilimali muhimu, na kuongeza ufahamu wa changamoto zinazowakabili.
Shirika la afya duniani WHO kanda ya Afrika kwa muda mrefu imekuwa ikikabiliwa na uhaba mkubwa wa wauguzi ambao, usiposhughulikiwa, unaleta tishio kubwa kwa maendeleo kuelekea huduma ya afya kwa wote.
Kulingana na makadirio ya hivi punde, kuna wauguzi na wakunga milioni 1.6 katika nchi 47 wanachama barani afrika.
Jumla ya 66% ya wauguzi wamejikita katika nchi sita – Algeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia, Ghana, Nigeria, na Afrika Kusini. Nigeria ndiyo inayoongoza kwa idadi kubwa ya wauguzi kwa asilimia 21, ikifuatiwa na Afrika Kusini kwa 18%.