Vijana kaunti ya Kilifi wahimizwa kupata mafunzo mafunzo ya kimaisha ili kuwa na ujuzi wa kujiajiri

Vijana katika kaunti ya Kilifi wameombwa kujitokeza na kupokea elimu ya miradi ya kiserikali inayolenga kuwaimarisha kiuchumi.

Akizungumza na Msenangu Fm rais wa bunge la vijana kaunti hii Jacinta Mbeyu Sanga anasema serikali ya kaunti na ile ya kitaifa imewekeza katika mipango ya kutoa elimu na pia mikopo kwa vijana kujiendeleza kupitia vikundi.

Also Read
Rais wa chama cha wanasheria nchini Nelson Havi amesema atang'atuka mapema wadhifa huo

Mbeyu  anasema ni wakati mwafaka kwa vijana wa eneo hili kukumbatia fursa hizi za kiserikali ili kujinufaisha kimaisha.

Also Read
Ipo Haja Ya Kuwahamasisha Wanaume Dhidi Ya Dhulma Za Kijinsia

Wakati huo huo Sanga amewataka vijana kujiandikisha katika mafunzo ya jinsi ya kujiendeleza na pia njia za kupokea mikopo inayotolewa na serikali.

Also Read
Wachimba Madini Wadogo Walalamikia Serikali Taita Taveta

Aidha vijana hao pia wametakiwa kutoa fikra ya kwamba ni sharti waajiriwe ndiposa waweze kufaulu maishani.

  

Latest posts

Gor Mahia Wapiga Kalamu Harrison na Benchi Lake La Kiufundi

Clavery Khonde

Sportpesa Yatoa Vifaa Vya Matibabu Kilifi

Clavery Khonde

Hospitali Za Kibinafsi Kukataa Huduma Za NHIF Mwezi Ujao

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi