Viongozi wa Kilifi Waunda Kamati Ya Kutatua Mizozo ya Ardhi

Viongozi wa kaunti ya Kilifi wakiongozwa na gavana wa kaunti hiyo Amason Jeffa Kingi na mbunge wa Magarini Michael Kingi wameongoza zoezi la kuundwa kwa kamati itakayoshughulikia suala tata la ardhi kwa wakaazi wa Kadzuhoni huko Magarini ikiwemo kukabiliana na bwenyenye anayedai kumiliki kipande hicho cha ardhi ili kuhakikisha wananchi hao wanapata hati miliki.

Also Read
Kampeni ya Kutoa Chanjo Kote Nchini Yazinduliwa

Suala zima la ardhi eneo hilo limekuwa donda sugu kwa miaka na mikaka ambapo hata ubomoaji wa majumba na uharibifu wa mali ushawahi shuhudiwa hapo.

Also Read
Makala: Njaa Yang'ata Kilifi

Kwenye mkutano huo kulifanyika uteuzi rasmi wa kamati mpya itakayofanya makubaliano na Bwanyenye wa eneo hilo ambayo pia ilipewa makataa ya siku thelathini kuhakikisha swala hilo linapata suluhu la kudumu.

Mshauri mkuu wa maswala ya sheria kutoka kaunti ya Kilifi Bibi Fondo, Waziri wa ardhi kitengo cha kaunti Maureen Mwangovya, mwakilishi wadi ya Gongoni Albert Kiraga na aliyekuwa Mbunge Wa Magarini Harrison Kombe ni miongoni wa viongozi waliohudhuria mkao huo.

Also Read
Kenya Breweries Yazindua Mvinyo wa Bei Nafuu

 

  

Latest posts

Uungereza Yaahidi Kushirikiana Na Kenya Kukabili Korona

Clavery Khonde

Wakenya Wahimizwa Kuwatunza Wanao Dhidi Ya Biashara Ya Ngono

Clavery Khonde

Viongozi Wa Dini Kwale Waonywa Dhidi Ya Kujihusisha Na Siasa

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi