Viongozi Wanaotoa Matamshi Ya Chuki Kutengwa

Wazee wa Kaya hapa Pwani wamesema kuwa viongozi wa kisiasa wenye wanakiuka maadili ya jamii katika uongozi wao huenda wakatengwa.

Katika kikao na wanahabari wazee hao wamesema baadhi ya viongozi eneo la pwani wamekua wakirushiana cheche za maneno majukwaani bila kuiheshimu jamii wanayoiongoza.

Also Read
Wanafunzi Kunufaika Na Masomo Ya Ziada Mvita

Kulingana na mshirikishi wa muungano wa wazee wa kaya Tsuma Kombe ni kuwa tayari wamepanga mikakati ili kuona kwamba viongozi hao wanaonywa dhidi ya mienendo yao katika uongozi.

Also Read
Wanasiasa Wasitumie Madhabahu Vibaya Wasema Viongozi Wa Dini Malindi

Kwa upande wake mmoja wa wazee hao Erastus Kubo ameelezea hofu yake ya kupotoka kwa maadili ya vijana katika jamii kutokana na  hulka za viongozi wa sasa.

Also Read
APTAK Yawahimiza Wananchi Kujiunga Kwenye Shirika Lao Ili Kuongeza Pesa Za Hazina

Aidha wametoa wito kwa viongozi wa eneo hilo kushirikiana ili kuleta maendeleo badala ya kuvutana na kutusiana hadharani.

  

Latest posts

Nitaiboresha Idara Ya Usalama Kaunti Ya Mombasa Asema Abdullswamad Shariff Nassir

Clavery Khonde

Mpango Wa Wanawake Wazinduliwa Kwlae

Clavery Khonde

Waziri Magoha Aahidi Uimarishwaji Zaidi Wa Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi