Viongozi mbali mbali wa kaunti ya Kwale wametuma risala zao za rambi rambi kufuatia kifo cha aliyekuwa mwakilishi wa kike wa kaunti hiyo Zainab Chidzuga.
Mwakilishi wa kike wa kaunti hiyo Zulekha Hassan ametoa pole zake kwa familia, marafiki na wakaazi wa kaunti hiyo kwa jumla.
Akizungumza na wanahabari, Hassan amesema kuwa habari za kifo cha Chidzuga aliyeugua ugonjwa wa corona zimempata na mshtuko mkubwa.
Kwa upande wake mbunge wa Msambweni Feisal Bader amesema kuwa kaunti ya Kwale imempoteza kiongozi shupavu katika masuala ya siasa na maendeleo.
Marehemu Zainab Chidzuga anazikwa adhuhuri hii ya leo huko kwao Golini Matuga.