Jumla vya vitambulisho 700 vya kitaifa kwenye eneo la Mokowe katika Kaunti la Lamu havijachukuliwa na wenyewe kutoka afisi ya usajili wa watu.
Hali hii inamanisha kwamba huenda watu hao wakakosa kusajiliwa kama wapiga kura endapo hawatavichukuwa kwa wakati unaofaa.
Eneo la Mokowe ni moja wapo ambayo yameathiriwa na visa vya utovu wa usalama katika siku za hivi karibuni.
Ikumbukwe kati ya mwaka 2014 na 2015 serikali isitisha shughuli ya kutoa vitambulisho vya kitaifa katika Kaunti ya Lamu kufuatia wasiwasi wa hali ya usalama ambayo ilisababishwa na magaidi wa Al-Shabaab.