Idara ya hali ya hewa imeonya kuwepo kwa kiwango cha chini cha mvua msimu wa vuli.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa tawi la Tana River imesema kwamba msimu wa mvua za vuli unatarajiwa kuanza mwezi Oktoba hadi mwezi Disemba.
Akizungumza afisini mwake mkurugenzi katika idara hiyo Kalu Guruba Nyale amesema kwamba maeneo yaliyoko karibu na ufuo wa bahari hindi kama vile Kipini,Witu Tarasaa na Tana Delta kwa Jumla mvua hizo zitaanza wiki ya pili ay a tatu ya mwezi Novemba na kutamatika wiki ya kwanza hadi ya pili ya mwezi Disemba mwaka huu.
Aidha amedokeza kwamba maeneo ya Galole pamoja na Tana Kaskazini mvua hizo pia zitakuwa za rasharasha na zitaanza wiki ya pili na ya tatu mwezi Novemba.
Amewataka wakulima hasa wanaotegemea mvua kupanda mbegu zinazomea haraka na kuwaonya kutarajia mavuno kidogo kutokana na uchache huo wa mvua.