#KurunziYaPwani
Chama cha waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte kimeshinda viti vingi vya ubunge kufuatia uchaguzi wa bunge wa nchi hiyo.Ushindi huo utamwezesha Rutte kubuni serikali mpya ya mseto ikiongozwa na chama chake cha VVD na pia kuhudumu kwa kipindi cha nne kama waziri mkuu wa nchi hiyo.Serikali yake ya mwisho ilijiuzulu mwezi januari mwaka huu kutokana na kashfa ya maslahi ya watoto. Rutte aliwashukuru wapiga kura nchini humo kwa kumpatia fursa nyingine ya kuongoza nchi hiyo.
previous post