Wafanyabiashara wa Kanda ya Afrika Mashariki Walalamikia Kupanda kwa Bei ya Mafuta Nchini

Mwenyekiti wa baraza la wafanyabiashara kutoka kanda ya afrika mashariki kimeungana na wakenya kulalamikia nyongeza ya bei za mafuta.

Aidha mwenyekiti wa baraza hilo Nicholas Nesbit amesema ipo haja ya wafanyabiashara kushauriana na serikali kuhusu namna ya kudhibiti bei za mafuta ili kupunguza gharama ya uzalishaji wa bidhaa.

Also Read
Je! Tanasha Donna Yuko Kwa Mahusiano na Msanii Omalay?
Mwenyekiti wa baraza la wafanyabiashara wa kanda ya Afrika Mashariki Nicholus Nesbit kwenye mahojiano na wanahabari mjini Mombasa

Nyongeza ya bei ya mafuta iliyotangazwa siku chache zilizopita itaathiri pakubwa shughuli za biashara katika kanda hii huku wafanyabiashara wengi wakipambana na athari za ugonjwa wa covid 19.

Also Read
Jamii ya Mijikenda yazindua mahakama za kitamaduni.

Nesbit aliyasema haya alipokutana na washikadau wa uchukuzi wa majini wakati ambapo bahari ya Kenya imetangazwa kuwa salama kwa vyombo kutia nanga, hii ni baada ya tahadhari ya awali kuhusu usalama katika maji ya kanda hii.

Also Read
Shehena Ya Kwanza Ya Chanjo Ya Korona Kuwasili Nchini Leo

Kwa upande wake afisa mkuu wa baraza la wafanyabiashara kanda ya afrika mashariki John Bosco Karisa amesema kuwa wanalenga kushirikiana na washikadau mbalimbali wa kibiashara katika kuimarisha utekelezwaji wa biashara kidigitali ili kupunguza kiwango cha ada wanazotozwa wanaposafirisha bidhaa.

Afisa Mkuu wa baraza la wafanyabiashara kanda ya Afrika Mashariki John Bosco katika mahojiano na wanahabari mjini Mombasa
  

Latest posts

Mshukiwa Mkuu Wa Mauaji Ya Mwanariadha Agnes Tirop Amekamatwa Mombasa

Clavery Khonde

Mbelle Awahimiza Vijana Kuzidisha Chachu Ya Talanta Zao

Clavery Khonde

Rais Kenyatta Amekutana Na Rais Biden Wa Marekani

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi