Wahudumu Wa Afya Wakosa Kazi Uingreza Baada Yakufeli Mtihani Wakiingereza Asema Waziri Kagwe

Wahudumu wa afya 10 kati ya 300 pekee ndio waliweza kupita mtihani wakiingereza kwenye mpango wa serikali wa kuwawezesha kuajiriwa na serikali ya Uingereza.

Haya nikulingana na waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe.

Also Read
Wizara ya afya yawaonya wakenya dhidi ya aina ya virusi vya Covid vya Delta

Akiongea katika kongamano lilowaleta maafisa wa afya nchini mjini Mombasa, Kagwe amewahimiza maafisa hao pamoja na wahudumu wa afya kuhakikisha wanajitayarisha vyema wakati wanapotakikana kusailiwa ili kuajiriwa kwenye mataifa ya nje

Aidha waziri Kagwe amesema serikali inalenga kuhakikisha kuwa maafisa wa afya humu nchini wanapata vibali vya kwenda kutoa huduma za afya kwa mataifa ya nje.

Also Read
Makundi ya kijamii Kilifi yamshinikiza waziri Kagwe kujiuzulu

Vilevile waziri wa afya ametoa onyo kwa maafisa hao kuhakikisha kuwa wanapata mafunzo ya kidigitali kama vile tarakilishi kwani operesheni nyingi za kiafya hivi sasa zinafanywa kwa njia ya kidijitali na huenda kutokuwa na ujuzi huo kukawakosesha nafasi ya kutoa huduma kwenye mataifa ya ughaibuni.

  

Latest posts

Uungereza Yaahidi Kushirikiana Na Kenya Kukabili Korona

Clavery Khonde

Wakenya Wahimizwa Kuwatunza Wanao Dhidi Ya Biashara Ya Ngono

Clavery Khonde

Viongozi Wa Dini Kwale Waonywa Dhidi Ya Kujihusisha Na Siasa

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi