Wakaazi wa Ganze wanazidi kutoa wito kwa wahisani kuelekeza misaada ya chakula na maji ya kunjwa katika eneo hilo ili kuwanusuru kutokana na makali ya janga la njaa. Wakaazi hawa wanasema hali inazidi kuwa ngumu mno kutokana na kiangazi kinachoendele.
Wakiongea na waandishi wa habari huko Bamba wanasema wanahofia hali hii ikizidi huenda hata wakapoteza maisha yao.
Wakaazi hao wanasema sasa wamegeukia kula mihogo pori ambayo wanasema imekuwa Atari mno kwa afya zao.