Wakaazi wa Mombasa Wahimizwa Kujichagulia Viongozi Bila Kushawishiwa

Mbunge wa mvita Abdulswamad Shariff Nassir amemtaka gavana wa Mombasa Hassan Ali Joho kuachia wananchi wa kaunti ya Mombasa kujichagulia viongozi wanao wataka hasa katika kiti cha ugavana.

Akiongea kwenye hafla ya boda boda katika eneo bunge la Jomvu alikoandamana na mbunge mwenza wa eneo hilo Badi Twalib amesema kuwa anashukuru gavana Joho kwa kuonyesha msimamo wa uongozi dhabiti.

Aidha Nassir amesema kuwa uamuzi wa uongozi uachiwe wakaazi wa eneo hili.

Kwa upande wake mbunge wa Jomvu Badi Twalib ameonya wale wanao tembea na vitabu kusajili wanachama mtaani kwamba hawana nia njema ila anadai ni kutaka kuharibu wanachama wa chama cha ODM.

  

Latest posts

Serikali ya kaunti ya Kilifi yatenga asilimia 15 ya bajeti kwa maendeleo

Joshua Chome

Kalonzo Aikosoa Serikali

Clavery Khonde

Rais Ruto Ateua Jopokazi Litakalo Tathmini Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi