Mgombea wa kiti cha ugavana katika kaunti ya Mombasa kupitia chama cha UDA Hassan Omar Sarai ameonyesha matumini makubwa ya kushinda kiti hicho cha ugavana kwenye uchaguzi wa Agosti 9
Akiongea katika hafla ya kumpokea rasmi aliyekua mgombea mwenza wa Suleiman Shahbal Selina Maitha katika makao makuu ya chama hiho mjini Mombasa [Sarai amesema kuwa wakaazi wa kaunti ya Mombasa wanatakiwa kubadilisha uongozi mbaya na kuwachagua viongozi waadilifu.
Wakati uo huo Sarai amesema lengo lengo lake kubwa ni kuleta uongozi bora ndani ya Mombasa na kubuni nafasi nyingi za ajira kwa vijana.