Wakazi wa Mkwakwani wanalilia haki.

Zaidi ya familia 500 kutoka kijiji cha Mkwakwani eneo la Ukunda kaunti ya Kwale wanalishinikiza shirika la ndege nchini la Kenya Airport Authority KAA kuwalipa fidia ya ardhi zao.

Also Read
Idara Ya Usalama Mombasa Yahimizwa Kuzingatia Utoaji Usalama Sawa Kwa Mirengo Yote Ya Kisiasa

Wakiongozwa na Kassim Choka, wakaazi hao wamemtaka rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati ili walipwe fidia ya ardhi zao ya shilingi bilioni 3 ili kutoa nafasi kwa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Ukunda.

Also Read
Viongozi Wakemewa

Aidha, wakaazi hao wamemlaumu pakubwa gavana wa Kwale Salim Mvurya na kamishena wa kaunti hiyo Karuku Ngumo kwa kuwatumia maafisa polisi wanaowahangaisha.

Also Read
Ruto Azuru Eneo La Pwani

Kutokana na hali hiyo, wenyeji hao sasa wameapa kutohama katika ardhi hiyo ya zaidi ekari 90 hadi pale watakapolipwa ridhaa yao na serikali.

  

Latest posts

Kiwango Cha Wateja Waliofurahia Huduma Za KRA Ndani Ya Miaka 3 Imeongezeka

Ruth Masita

HURIA Yalaumu Vyama Vya Kisiasa

Clavery Khonde

Wakaazi Kwale Waitaka Serikali Kushughulikia Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi