Licha ya visa vya korona kuongezeka humu nchini wakenya wengi bado wanaendelea kupuuza maagizo yaliyowekwa na wizara ya afya ili kudhibiti msambao wa virusi hivyo.
Kulingana na wizara ya afya nchini, kuvaa barakoa, kunawa mikono mara kwa mara na kuweka umbali wa mita moja ni baadhi ya njia za kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo hatari ila kwa wakenya wengi hawafuatilii tena maagizo hayo.
Kulingana na wakaazi wa Likoni, wanasema serikali haitilii maanani kuhakikisha kwamba kuna vifaa vya kutosha vya kusaidia wananchi kuweza kujikinga na virusi hivyo,kwani mifereji na mabomba yaliyokuwa yamewekwa awali katika kivuko cha ferry cha Likoni ili kusaidia wakenya waweze kunawa mikono kabla ya kuvuka kwa sasa haitoi maji tena na wengi wao wamelalamikia hali ya uchumi ambayo imezorota na kuwafanya wakose hata senti ya kununua barakoa.