wakili George Kithi anasema sheria ya umiliki wa mashamba inafaa kubadilishwa

Baadhi ya Mawakili katika ukanda wa Pwani wamesisitiza haja ya kufanyiwa kwa masekebisho ya sheria za umiliki wa ardhi nchini.

Wakiongozwa na Wakili George Kithi, mawakili hao wamesema mfumo unaotumika kwa sasa wa umiliki wa ardhi unazidi kuwakandamiza wakaazi wa Pwani hasa kaunti ya Kilifi.

Also Read
Waathiriwa Wa Bwawa La Mwache Kufidiwa

Akizungumza katika eneo la Shariani kaunti Kilifi, Wakili Kithi amesema kufanyiwa kwa marekebisho kwa sheria hizo kutasitisha mizozo ya ardhi pamoja na kulikabili swala la uskwota hapa Pwani.

Also Read
Jux kwenye Tamasha la wanawake

Hata hivyo amewarai wakaazi wa eneo la Shariani na kaunti nzima ya Kilifi kuunga mkono azma yake ya kuwania kiti cha useneta kaunti ya Kilifi akisema mabadiliko mengi ya uongozi huchangiwa na viongozi waadilifu.

  

Latest posts

Mshukiwa Mkuu Wa Mauaji Ya Mwanariadha Agnes Tirop Amekamatwa Mombasa

Clavery Khonde

Mbelle Awahimiza Vijana Kuzidisha Chachu Ya Talanta Zao

Clavery Khonde

Rais Kenyatta Amekutana Na Rais Biden Wa Marekani

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi